LATEST POSTS

Thursday, August 27, 2015

AROBAINI (HITMA)YA BANZA STONE


                         AROBAINI YA BANZA STONE

Arobaini ya nyota wa Muziki wa dansi Nchini Tanzania Ramadhani Ally Masanja maarufu kama Banza
Stone imefanyika Siku ya Jumapili iliyopita ya Tarehe 23 Agost 2015  Nyumbani kwao Sinza Kijiweni na kuhudhuriwa na wapenzi na mashabiki wa nguli huyo pamoja na Ndugu,Jamaa na marafiki.
                     

                        

Akiongea na Kavasha,Kaka wa Marehemu Banzqa Ndugu Jabir Masanja amesema anawashukuru watu wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kumuuguza marehemu Banza Stone hadi mauti yalipomkuta kwani ahadi ya kumrejea Mungu wake ilifika na kamwe haina kizuizi.

Mwalimu wa walimu Banza Stone alifariki Siku ya Ijumaa Tarehe 17 Agosti 2015 saa 7 mchana baada ya kuugua kwa vipindi tofauti tofauti na kutibiwa katika Hospitali za Palestina na Mwananyamala Jijini Dar-Es-Salam.

Marehemu Banza alizikwa siku ya Jumamosi Tarehe 24 Agost 2015 katika makabuli ya Siza Jijini Dar-Es-Salaam.


                             Marehemu ameacha mtoto mmoja Hajji Masanja.

            BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIHIMIDIWE 
                   REST IN PEACE RAMADHANI MASANJA''BANZA STONE'' 

0 comments:

Post a Comment