LATEST POSTS

Saturday, June 18, 2016

UHUSIANO WA MUZIKI NA HISABATI BY LISTER ELIA

MUZIKI NA HISABATI NI NDUGU WA KUZALIWA TUMBO MOJA.
PATA UFAHAMU WA ALAMA, MICHORO NA MAANDISHI YA KI-MUZIKI.
Imeandikwa na Lister Elia -www.listerelia.com.

Alama, michoro na maandishi ya ki-muziki(staff-notation),notes(noti) au kama wengine waitavyo "nota",ni mfumo ambao unamuwezesha mtu kuhifadhi wimbo alioutunga katika maandishi ili kuwawezesha wengine kuupiga au kuiga wimbo wake kufuatia maandishi hayo maalum.
Mfano,ni kama viongozi wa nchi wanavyopigiwa nyimbo za mataifa yao popote waendapo katika safari za kikazi.Ni kwasababu nyimbo za mataifa yote,notes zake zimeandikwa ili zisomeke na wanamuziki waliojifunza maandishi na alama hizo maalum.
Leo ningependa kuainisha hizi alama,michoro/maandishi maalum ili kuwapa ufahamu haswa wadau wa muziki ambao wangependa kufahamu hii michoro,alama... maana yake na thamani zake.
Hapa sintozungumzia maelezo ya vitendo(practical),nia ni kusambaza ufahamu wa juu juu tu.
Tuangalie michoro kama unavyoiona,kielelezo(hapo chini) kinavyoonesha.
Noti ya kwanza ambayo ina umbo la yai inaitwa SEMIBRAVE au WHOLE NOTE,ina thamani ya mapigo manne.
Noti ya pili yenye umbo la yai lenye mkia inaitwa MINIM au HALF NOTE na thamani yake ni mapigo mawili.
Noti ya tatu inaitwa CROTCHET, au "a Quater note", ambayo umbo lake ni la yai lenye giza na mkia,ikiwa na thamani ya pigo moja.
Noti ya nne inaitwa QUAVER au ONE EIGHTH NOTE,umbo lake ni YAI lenye mkia wa kibendera uliojikunja kwa juu,thamani yake ni "moja ya 8".
Noti ya 5 ni SEMIQUAVER au "A SIXTEENTH NOTE",umbo lake ni yai lenye giza na mikia ya vibendera viwili.Thamani
yake ni "moja ya 16."
Bado kuna noti nyinginezo  lakini hizo ndizo noti za msingi.

Ukijifunza namna ya kusoma na kuandika notes,inakuwa rahisi kwako kujichanganya na wanamuziki wa ki-mataifa na zinafanya usiwe na kikomo katika ufahamu wa muziki.
Wale ambao hatujasoma muziki tunatumia zaidi sikio na memory,lakini kuna miziki ambayo huwezi kuisikiliza tu na kukopi kama Classical au Jazz kwani ufundi wa kisomi ni mwingi sana.

0 comments:

Post a Comment