Mwanamuziki Elibariki Zacharia Kunukula.
Kwa mara nyingine Kavasha blog inakuletea mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi akiwa ni mtunzi,mwimbaji na mpiga kinanda kwa uwezo mkubwa kabisa,si mwingine bali ni Elibariki Zacharia Kunukula ambae tumeweza kuzungumza nae mengi yahusuyo familia yake,kazi yake ya muziki na mengine mengi yahusuyo tasnia hii,kwa ufupi kabisa nakuletea sehemu ya mahojiano hayo na mgeni wetu Elibariki ambae alianza kwa kujitambulisha;
Elibariki Zacharia Kunukula.
Naitwa Elibariki Kunukula,ni mzaliwa wa
Mkoa wa Singida katika kabila la Wanyiramba,alianza muziki mwaka 1998 Mjini
Arusha na Bendi yake ya kwanza ilikua ikijulikana kwa jina la The Ambassadors
Band,Muda si mrefu Bendi hiyo ilivunjika na nikaitwa Moshi kwenda kuanzisha
Bendi iliyojulikana kwa jina la Rhino FM ambayo haikudumu na baade kutimkia
Tanga nilipoalikwa kujiunga na Bendi ya Fax Jazz Band ambapo nilidumu kwa muda mrefu sana nikifanya
kazi na wakongwe kama vileSteven Hizza, Ziggy Saidi na Marehemu Hassan Ngoma
Hawa ni wakongwe wa Bendi kongwe ya Mjini Tanga hapo zamani iliyojulikana kama
ATOMIC JAZZ wakiwa pia na Mzee Mganga
ambaye ni Baba yake mzazi wa Kassim
Mganga huyu nyota wa Bongofleva hadi alipokuja Ally Choki kunichukua kujiunga
na Extra Bongo ya Jijini Dar Es Salaam.
Muimbaji wa Utalii Bendi ELIBARIKI KUNUKULA.
Pale Extra Bongo sikukaa sana nikapata kazi
kwenye mtandao wa Hotel ziitwazo Nyumbani Lounge Hotels & Resort zilizopo
Tanga na Moshi mkoani Kilimanjaro nilipokua nikipiga sequencer muziki wa mtu mmoja (jeshi la mtu
mmoja) baada ya mkataba kwisha niliitwa na Profesa mmoja wa UDSM kuanzisha
Bendi yake ambayo hakudumu kutokana na Profesa huyo kuwa hakujipanga ipasavyo
kuanzisha Bendi,hapo ndipo nilipochukuliwa na Utalii nikiwa kama mtu wa sequencer
baadae wakaja Ramadhani Kilindi na
Duncan ndumbaro wakanikuta nikipiga peke angu ndipo ulipoamua kuifanya kuwa
Bendi hapo ndio mwanzo wa Utalii Bendi hii tuliyonayo sasa.
Le Grande Utalii Band
Bendi yetu inapiga nyimbo
mchanganyiko,tunapiga kopi za aina zote kadiri tunavyozifanyia mazoezi ingawa muziki aina ya Kavasha ndio
kipaumbele chetu,pia tuna nyimbo zetu wenyewe tulizorekodi na zinapigwa redioni
tumeshafanya video zake ambazo tutaziachia hivi karibuni.
Kuhusu albam tumejiandaa kuzindua albam
yetu siku ya Tarehe 4 Septemba 2015
tunawaomba wapenzi wa muziki wa dansi
wote hususani wa Utalii Band
kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo kwani tumewaandalia mambo mazuri
si ya kukosa kwa kweli.
Elibariki (kulia)akiwajibika jukwaani.
Muziki mwingine aina ya Taarab unapigwa na
kundi letu pacha la Utalii Bendi kwa maana kuwa kunakundi hili nililopo la
muziki wa dansi linalojulikana kama Le Grande Utalii Band na hilo jingine
linajulikana kama Utalii Taarab.
Suala la kuhamahama kiukweli linatokana na
kutafuta maslahi na wakati mwingine ni kwa wanamuziki kushindwa kustahimili
ukata pindi unapoingia kwenye Bendi Fulani.Na suluhisho la hili ni kwa Wamiliki
wa Bendi kujiandaa vya kutosha kabla ya kuanzisha Bendi,pili ni kuwapa mikataba
ya kueleweka ya ajira ya kueleweka kabla ya kuanzisha Bendi ili waache
kututumikisha kama Big G ambayo ukiitoa dukani ni tamu lakini ukiitafuna baada
ya muda inaisha utamu unaitema na kuitupa,Lakini pia yatupasa wanamuziki
tujitambue kwani ujuzi wetu una thamani kubwa mno.
Kundi zima la Utalii Band wakiwajibika jukwaani.
Kuna baadhi ya Bendi hutoa mikataba naomba
kwa kweli tuiheshimu mikataba hiyo ingawa wakati mwingine wamiliki wa Bendi
hutoa mikataba minono wanapokuhitaji ila unapofika kwenye bendi husika
hutekelezewi baadhi ya mahitaji muhimu yaliyoainishwa katika mkataba husika,na
hata hali ikiwa hivyo unashindwa kuondoka kwa kuwa unalazimika kuilipa Bendi hali
ya kuwa hujatimiziwa mahitaji yako lakini ulishasaini mkataba na pesa ya kurudisha huna hapo unabaki na
stress kibao hadi atokee tajiri mwengine akupe mkataba na pesa urudishe kule
uende huku,unazunguka mule mule ingawa wengine wanashindwa kurudisha na kuzua
tafrani.
Katika muziki nimepata mafanikio mengi sana
ingawa sijapendelea kuyaweka wazi ispokua kikubwa ni kukuwa kwa kasi kubwa kwa
kiwango change cha ujuzi wa muziki kwani tofauti na kuimba pia ni mpiga kinanda
wa kiwango cha juu na hata Extra Bongo niliitwa kwa sababu ya kuwa mpiga
Kinanda.
Le grande Utalii band inaundwa na
wanamuziki wafuatao;
Waimbaji ni- 1.Elibariki Kunukula
2.James Mulamba na
3.Ramadhani Kilindi
Magitaa ni – 1.Omar Seseme-SOLO
2.Duncan Ndumbalo-RHYTHM
3.Juma Zegezo-Bass
Kinanda-Yupo Emma Mabele
Drums yupo
Steven Muzenga
Kundi la Utalii Bendi likifanya yao.
Awali tulikua na Komandoo Hamza Kalala
ambaye kwa sasa amejipumzisha na huwa anakuja siku moja moja kutupa kampani,tulikua
pia na Rashid Sumuni ambae kwa sasa ameondoka moja kwa moja.
Kundi la pili La Utalii Taarab lina
wanamuziki wafuatao
Waimbaji wakiume ni-1.Mwinyimkuu
2.Chai ya Rangi
3.Melody Totoo
Waimbaji wa kike ni -1.Maina
2.Poke
3.Zulfa
Kinanda yupo- Moshi Hamisi Sentee
Drums yupo Fadhili.
Utanashati ni jambo la lazima kwa mwanamuziki anaejitambua.
Katika familia yetunaweza kusema ni familia
ya muziki,wadogo zangu wote ni waimbaji ingawa kwa sasa wanaimba kwaya lakini
kwa kiwango cha juu kabisa,Baba yangu nae alikuwa mwimbaji mzuri sana na
alikuwa akifundisha kwaya ya Shuleni kwake kwani alikua ni Mwalimu,yeye nae
alirithi kutoka kwa baba yake ambae alikua na kipaji kikubwa cha kuimba na
kupiga zeze kwa ustadi wa hali ya juu.
akirekebisha vyombo ili mambo yaende vizuri
Jambo kubwa ambalo siwezi kulisahau
maishani ni kuondokewa na Baba yangu mzazi mzee Zacharia Kunukula mnamo Tarehe
23/05/2011 ambaye ukiachilia mbali ya
kifamilia lakini pia alikua mhimili wangu mkubwa kimuziki na alinisaidia
sana kufika hapa nilipo.
Mwisho natoa ushauri kwa wanamuziki
wenzangu tupendane,tushirikiane kwa kuyafanya haya tunaweza kkuirudisha hadhina
heshima ya muziki wa dansi kurudi kama zamani na tuache kudharauliana kuwa huyu
anajua na huyu hajui hapo hatujengi bali tunabomoa.
Elibariki katika pozi.
Asante sana wana Kavasha kwa mahitaji ya
kufahamu Bendi yako ya Utalii ilipo,inafanya nini nautaipata vipi kwa muda
upi,ama kwa kunihitaji mimi mwenyewe kikazi zaidi ama kwa maelezo zaidi
Wasiliana name Elibariki Zacharia Kunukula kwa;
SIMU
NAMBA +255715606171
EMAIL ADRESS-kunukulaelibariki@gmail.com
Kavasha Group inakupa pole kwa kuondokewa na Baba na nguzo yako Mzee Zacharia Kunukula,tunaomba Mwenyezi Mungu amuweke mahali pema peponi Amen .
Safi sana
ReplyDeleteSafi sana
ReplyDeleteNamkubali sana kunukula katika kazi.
ReplyDeleteUtalii band iko vzr
Ila msibweteke.
anajijua yupo vzr
ReplyDelete