BIMA YA AFYA
Kundi
wanza la wanamuziki waliojiandikisha kujiunga katika mpango wa Bima ya
afya,linatarajiwa kuanza kupata huduma hiyo rasmi kesho Tarehe 21 August 2015 katika
ofisi ya BASATA Jijini Dar-Es Salaam ambapo watapatiwa Kadi zitakazowawezesha
kupata huduma ya matibabu katika Hospitali zote kubwa za Serikali na baadhi za
Binafsi kama vile Regency nk.
NDUGU JOHN KITIME;Kiongozi wa Mtandao wa Muziki Nchini.
Akiongea na Kavasha,Kiongozi wa Mtandao wa
Muziki Nchini Anko John Kitime amesema kuwa
mpango huo umeratibiwa na Mtandao wa Muziki nchini kwa kushirikiana na
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini NHIF na kwamba Mwanamuziki atalazimika
kutoa kiasi cha Tshs 96800/= ambayo itamuwezesha kupata huduma hiyo kwa mwaka
mzima .
ANKO JOHN KITIME''Wanamuziki tujitokeze kwa wingi kwa ajili ya afya zetu''.
Anko Kitime ameongeza kuwa kiasi hicho ni
kidogo kulinganisha na gharama halisi ya matibabu ambayo hayana dhamana yoyote
ile,amewashauri viongozi wa vikundi vya muziki na wanamuziki wenyewe kujitokeza
kwa wingi ili kupata huduma hiyo.
NDUGU FRESH JUMBE''Kama itaruhusu kuchukua dawa katika maduka
ya madawa itakua nzuri sana''.
Amesema kuwa Mtandao anaouongoza umefanya
juhudi kubwa kuunganisha Mfuko huo wa Bima na Wanamuziki ili kujaribu kusaidia
wanamuziki hao pale wanapofikwa na maradhi kwani huwa katika wakati mgumu
kutokana na baadhi yao kutomudu gharama
za matibabu pale wanapokuwa hawawezi kufanya shughuli yao hiyo.
Venance Geuza(Anko Vena)''Ni fursa nzuri ambayo tuliitafuta kwengine''.
Wakiongea na KAVASHA kwa nyakati
tofauti,Baadhi ya wanamuziki wamesifu mpango huo na kusema umekuja wakati
ukihitajika,wanamuziki hao ni Musa Karenga, Fresh Jumbe,Elibariki Kunukula na
Venance Geuza ambae alisema ni mpango mzuri na viongozi wahakikishe umefanikiwa
kwani wapo wengine walitoka katika muziki na kwenda kuajiriwa kwenye sekta
rasmi ili kupata huduma hiyo ya Bima ya Afya.
KAVASHA inawatakia kazi njema na kuwaomba mjitokeze kwa wingi kupata huduma
hiyo muhimu na adhimu.
0 comments:
Post a Comment