LATEST POSTS

Showing posts with label KAVASHA GROUP TANZANIA. Show all posts
Showing posts with label KAVASHA GROUP TANZANIA. Show all posts

Tuesday, February 23, 2016

MAHOJIANO KATI YA KAVASHA GROUP NA M-TANZANIA ,JAZZ PIANIST/AUTHOR, LISTER ELIA.

Leo tuna mgeni ambaye ni mtanzania aishiye na kufanya kazi mashariki ya mbali kule nchini Japani,si mwingine bali ni ndugu yetu Lister Elia ambaye anafahamika sana kwa uhodari wake wa upapasaji wa kinanda,Kavasha ilifanya nae mazungumzo na ilikuwa kama ifuatavyo;                
                                                           Ndugu   Lister  Elia.

1.Habari yako kaka Lister,watanzania na wote wasomao blog yetu ya Kavasha wangependa kujua historia yako japo kwa kifupi.

Lister anajibu;Nashukuru kwa kunikaribisha katika jamvi hili tukufu la KAVASHA,kitaaluma mimi ni Pianist/Keyboardist na pia ni mwandishi wa vitabu,hadi sasa nimeandika vitabu vitatu ambavyo ni 1.Jifunze Gitaa,2.Jifunze Piano na ‘’The mystery of Tamko’s death" ambacho ni cha riwaya.

Nilisomea masomo ya awali ya muziki kule Bukoba katikachuo kiitwacho Ruhija Musical Academy,elimu ya kati ya muziki kule Vienna Austria na elimu ya juu ya muziki nimesomea katika chuo kiitwacho Mate School of Music kilichopo Jijini Tokyo Japani.
Pamoja na kupiga muziki kama mwanamuziki wa kulipwa,lakini pia nafundisha muziki katika vyuo mbalimbali vya muziki Japani kama njia nyingine ya kujiongezea kipato,nilianza kupiga kinanda tangu nikiwa na umri wa miaka 6 kwani kinanda kilikuwa kwenye anga zangu wakati wote kwa nia kujifurahisha tu na sikujua kama ndiyo itakua shughuli yangu kuu siku za baadae kama ilivyo sasa.

Wasifu wangu na mengine mengi yanapatikana kwenye tovuti yangu ambayo ni www.listerelia.com

2.Kavasha ikamuuliza ni lini alianza kujishughulisha na shughuli za muziki?

Lister anajibu;Shukrani za kipekee zimfikie Kikumbi Mwanza Mpango ‘’King Kikii’’,yeye ndiye aliyenishawishi kupiga dansi katika bendi yake kwa mara ya kwanza katika Bendi yake ya King Kiki Double O Orchestra,Baadae nilikuwa kiongozi wa bendi iitwayo Benebene Group,tulipiga zaidi katika mahoteli ya kitalii... zaidi tukipiga katika Hotel ya Kilimanjaro ukumbi wa Tanzania Room kama uwanja wa nyumbani.
                                     Mzee Kikumbi Mwanza Mpango-King Kik

Bendi yangu ya tatu ilikuwa Sambulumaa ambapo nilipiga nyimbo kama Kadiri mke wangu na CCM imekua zilizotikisa sana anga la muziki wa dansi miaka hiyo’’sikiliza nyimbo hizo katika….. https://youtu.be/JPvLxCSeLIU na https://youtu.be/p7DihqWrr8

Bendi yangu ya nne ilikuwa OSS Ndekule na ya mwisho nchini Tanzania kabla sijaelekea nje ya nchi ni bendi ya MK Group maarufu kama wana’’ Ngoma za Maghorofani’’,hapo nilipiga na kurekodi nyimbo lukuki mojawapo ni Maumivu Makali utunzi wa marehemu Joseph Bartholomew Mulenga ipo hapa https://youtu.be/4gbuerY3Fv4

3.Je Uliondoka lini na ulianza anzaje muziki ughaibuni?

Lister anajibu;Niliondoka Tanzania mwaka 1991 nikiwa na mipango ya kwenda Paris,Ufaransa kufanya kazi kama mwanamuziki wa kulipwa,mdhamini wetu alikuwa mwanamke Mfaransa mwenye asili ya Israel ambae aliamua tupige kambi jijini Nairobi Kenya kabla ya kuelekea Ufaransa.Nikiwa hapo Nairobi,safari ya kuelekea Japan ilijitokeza kwanza hivyo,nilibadili mawazo na kuelekea Mashariki ya mbali badala ya kwenda Ulaya.


                                         Lister akiwa safarini kikazi na wenzake.

4.Ni wanamuziki gani na bendi gani ambazo ulifanya nazo kazi huko nje ya Nchi?

Lister anajibu;Nimefanya kazi na wanamuziki wengi wa kimataifa toka nchi mbalimbali,majina ni mengi mno na bendi ni nyingi mno ila,la muhimu ni kwamba pamoja na kupiga miziki ya kwetu na ya wengine,ninalo kundi langu,tunapiga Jazz music kwenye matamasha mbalimbali kama unavyoweza kuona hapa…. https://youtu.be/G2ZKsHYc5yU na unaweza kuona live concert kwenye tamashala live la Jazz Tokyo hapa…. https://youtu.be/tZEPJ42hvNM

5.Ni vikwazo na changamoto gani ulikumbana navyo huko Japan wakati ukianza kazi yako huko Japan?

Lister anajibu;Changamoto ni nyingi na zote zilihusiana na maisha ya ugenini kama vile;

(a).Lugha-Mwanzo ilikuwa vigumu kwani wa-Japani hawaongei Kiingereza mpaka nilipoijua lugha yao changamoto nyingi zikaanza kupungua.

(b).Maandishi yao yako based on characters na si alphabet hivyo kujifunza hizo characters za kanji,katakana na hiragana zimenichukua miaka mingi ya kujifunza.

(c)Ubaguzi wa rangi bado upo-upo Duniani na Japan haina tofauti na nchi nyingine japo,miaka ya karibuni kwenye miji mikubwa ubaguzi unaelekea kutoweka ama kupungua taratibu.


                                                                 Akiwajibika jukwaani.

6.Je unaonaje maendeleo ya muziki wa dansi nchini Tanzania?

Lister anajibu;Maendeleo ya muziki wa dansi Tanzania naona ni ya kusua-sua kwani ile enzi ya wanamuziki ‘’kukuna vichwa kwa ubunifu’’imetoweka,kuiga muziki wa chi jirani kumeshamiri,bendi karibu zote zinapiga muziki unaofanana na si rahisi kupambanua bendi hii na ile ,kukosekana kwa ubunifu kumefanya hata wapiga vyombo kuiga style ya Wenge Musica na hivyo kuwa na miziki isiyo na rangi tofauti na bendi nyingine.

7.Ni bendi ipi na mwanamuziki yupi anayekuvutia Tanzania?.

Lister anajibu;Binafsi napenda kuangalia na kujifunza kutoka kwa’’ wanamuziki wa kimataifa’’ kuliko kuangalia wanamuziki wa nyumbani kwani nilitoka kitambo kwenye ‘’daraja la kitaifa’’ kwani kwa kiwango cha muziki wa nyumbani Tanzania,kama yapo ya kujifunza ni machache,hivyo nguvu zangu nimezielekeza kwenye ‘’ jukwaa la kimataifa’’ na wanamuziki wa kimataifa’’. 
                                                                Akivicharaza vinanda.
 
 8.Baadhi ya wanamuziki wa dansi nchini Tanzania nidhamu yao inaonekana kushuka siku hadi siku,unalionaje suala hili?

Lister anajibu;Nilikuwa nyumbani kipindi fulani mwaka jana / juzi,nilizunguka kuziona bendi karibu zote kubwa,niliona utovu mwingi wa nidhamu jukwaani,mfano baadhi ya wanamuziki kuchelewa kuingia jukwaani,kuitaita majina ya wateja katika hali ya kuwapandisha mori ama kuwahamasisha wateja hao watoe kitu,kuvuta sigara,kuongea na simu wakati mazoezi yakiendelea na mengine mengi yafananayo na hayo ambayo hayafai kwa kazi yetu ya muziki hususan wa dansi.

9.Unatarajia kurudi lini nyumbani kufanya shughuli zako za muziki ukiwa katika ardhi ya nyumbani?

Lister anajibu;Sina matarajio ya kurejea nyumbani hivi karibuni,kwani hakuna uhaba wa kazi nilipo,kama kurudi, nitarudi panapo majaliwa ya mwenyezi Mungu lakini si kesho wala keshokutwa.

10.Unadhani kuna sehemu ambayo unaona serikali inaweza kusaidia kuinua muziki?kama ipo ni ipi?

Lister anajibu;Kwenye mahojiano yangu mengi na vyombo vya habari TZ,nimependekeza mara nyingi kuwa serikali inatakiwa kuanzisha masomo ya muziki kwenye mitaala ya shule za msingi,elimu ya muziki haipo Tanzania na hivyo kupelekea matumizi ya vipaji pekee.

*Vipaji vikipaliliwa na elimu matokeo yatakuwa bora zaidi,vipaji pekee vinakuwa na ukomo* hasa kama mwanamuziki anataka kuwa na kiwango cha ki-mataifa.

                           Hii ni katika live concert katika Jiji la Tokyo nchini Japan.


11.Unawashauri nini wanamuziki na wadau wa muziki nchini?

Lister anajibu;(a)Kwa wanamuziki ni kwamba tujenge tabia ama mazoea ya kujisomea vitabu vya muziki na kujiendeleza zaidi kitaaluma .

(b)Kwa wadau-Tujifunze kuzikosoa tabia zisizopendeza za *BAADHI* ya wanamuziki kama kuomba-omba mahali pa kazi pia kuzikosoa kazi zao pale tusipofurahishwa,itakuwa changamoto nzuri na hao wanamuziki BAADHI watashituka na kuchukua hatua kujirekebisha kitabia na kikazi.Hapa nasisitiza "SI WANAMUZIKI WOTE WENYE KASORO HIZO".

12.Kaka Lister Elia tunakushukuru sana kwa muda wako,tunakushukuru sana kwa maelekezo yako kwa serikali,wadau na wanamuziki,karibu sana na usisite kutoa ushirikiano pale tutakapokuja kukuomba taarifa yoyote inayohusu muziki na maisha.

Lister ;Shukrani kwa kunikaribisha kwa pamoja tutalisukuma gurudumu la kavasha lisonge mbele.
                                      

                         KAVASHA GROUP YAKUTAKIA MAISHA MEMA NA KAZI NJEMA.





Monday, September 21, 2015

MARTIN KIBOSHO;UVUMILIVU NA KUJITUMA NDIO KILA KITU KATIKA MUZIKI,SEHEMU YA 1.


        SAFARI YA KIMUZIKI YA MARTIN KIBOSHO.


Mwenyewe anasema;

                                               Martin Kibosho akiwa kazini.

Nilianza muziki Mwaka 2000,nilianza na Mand inaitwa Muungano nilikua kama drummer chipukizi nilikua na mpiga drums maarufu anaitwa kang’ombe kwa sasa yuko Msondo Ngoma Music nilikaanae kwa muda wa miezi 6 akiwa ananionyesha vitu fulani,baada ya hapo nikatoka kwenda African Beats kwa mzee Mafumu Bilali nilikaa mwaka 1 nikatoka nilipita viband vingi sana vidogovidogo wakati mwingine na mdogo wangu James Kibosho ila yeye alidumu sana na Bendi ya The African Stars''Twanga Pepeta''kabla ya kutoka hivi karibuni.

 

                                       Vipaji Band Jukwaani Nchini Ufaransa.

Viband nilivyopita baada ya hapo ni Tango Stars,Wasi Musica,Nina musica,Santon Band, Zote nilikua napitapita tu ili nipate ujuzi zaidi kitu nilichofanikiwa hadi kufikia Bendi zilikoa kubwa nchini kama Twanga Chipolopolo nilipiga album yote ya ''hujafa hujasifiwa''na Extra Bongo 3x3 na Mtenda akitendewa,African Revolution''wana TamTam''Mchinga Sound''wana TimbaTimba'' chini ya Ally Choky tukarekodi albam ya''Mwaka wa Tabu'' zikafatia safari za Dubai na Muscut kupiga kwa mkataba miziki ya kopi na hatimae kwenye Band hii niliyonayo huku Australia ambayo tunapiga mizki mbalimbali ya kiafrika na Dunia kwa ujumla ikiwepo ya kusindikiza michezo ya sarakasi nk

                             Kundi la wanasarakasi wanaoshirikiana na Vipaji Band. 
Band  hii  inaitwa Vipaji ambapo kuna wanamuziki  kama Martin Kibosho,Kado Bass,Moses  Mpiga Saxophone,Kuna Dr  Kumpeneka anaimba na kupiga percussion kuna Maneno Uvuruge mpiga guitar, kuna Tom Nigura mpiga keyboard  na wa mwisho ni kiongozi wetu Bob Rudala nadhani ni majina maarufu katika tasnia ya muziki wa dansi nchini Tanzania,Pia kuna mwimbaji wa kike kutoka zimbabwe anaitwa Seletemba .

                                                                 Vipaji Band.
 Tumezunguka na Vipaji Band sehemu mbalimbali Duniani na kwa sasa napenda wasomaji wetu uwawekee show yetu ya nchini Ufaransa ambayo ni moja ya Tour ndefu na yenye mafanikio makubwa.


                             Foleni ya kuingia kwenye show ya Vipaji Band Jijini Paris.
 Hiyo Show tulifanya Ufaransa Mjini Paris,ni show kubwa sana hapo kuna mataifa manne, tuko sisi watu wa Band wote ni watanzania kuna group kutoka Ethiopia,Zimbabwe na South Africa,hapo sisi kazi yetu ni kupiga music laini, tunapiga muziki tofauti style zote kiafrika ndio sana kizungu kidogo coz hiyo ni show ya kiafrika

Ilikua mwaka jana ambapo  tulifanya show mjini Paris mwezi mmoja baadae  tukaanza  tour ya mikoani tulizunguka Miji 22 Nchini Ufaransakwa u jumla wake ambapo ilitufikisha mpaka Uswisi  jumla tulikaa miezi mitatu.


              Kiongozi wa Kundi hilo Bob Rudala akiwa na wacheza Sarakasi wa kundi hilo.
 
Dr.Kumpeneka,Maneno Uvuruge,Martin Kibosho,Moses Saxophone,Tom Keyboard,Kiongozi Bob Rudala na Kado Bass.



Tuangalie picha mbalimbali kuona yale yaliyojiri katika ziara hiyo ya Ufaransa,Tour de France;



                                                   Paris,France.

 
                                                      Paris,France.

 
                                                        Paris,France.

                                                    Paris,France.

                        
                                                    Paris,France.

                                                            France.
                                                  France.

 
                                                      France.

                       
                                                  France.
                                             France.

 
                                             In France.
 
                                                 France.
           
                                              Kado Bass akiwajibika.

 
                                                 France.
 
                    Martin akiwa na wapiga ngoma Mjini Paris Ufaransa.

 
                                            France

 
                                                      France.

                      
                                                       France.

            
                                              Martin Mzigoni.
 
                                                France.

Friday, September 18, 2015

THE GRAND UTALII BAND YASIMAMISHA MADANSA WAKE WOTE

               THE GRAND UTALII BAND YASIMAMISHA WANENGUAJI WAKE.

        Waliokua wanenguaji wa Utalii Band wakiwa kazini kabla ya kusimamishwa.

 Bendi ya Utalii ya jijini Dar-Es-Salaam imewasimamisha kazi wanenguaji wake kwa wote kutokana na gharama za uendeshaji ambapo awali Bendi hiyo ilikua na makundi matatu ambayo ilikua ni The Grand Utalii A,The Grand Utalii B na The Grand Utalii Taarab,zoezi hilo litahusu kupunguza na wafanyakazi wa Bendi hizo na kuimarisha Bendi moja na ambayo itaweka mfumo wa ajira ya kudumu.

                Hapa ni mambo ya kusebeneka na Utalii Band.

Taarifa za awali zilizoifikia Kavasha Blog zilisema kuwa baadhi ya wanenguaji hao waliaga kwa matatizo ya kifamilia lakini walionekana kwenye majukwaa ya Bendi tofauti jambo lililoukera uongozi wa Grande Utalii Band na hivyo kuamua kuwatimua kazi,awali Bendi hiyo ilikua na wanenguaji sita ambao ni Chiku Kacka,Flolah Bambucha,Vero,Regina,Salma na Otilia Boniface,ambao kati yao inasemwa na chanzo chetu kuwa Otilia yupo na Bendi ya TOT katika kampeni,Regina na Salma wamerudi Double M Sound,Vero yupo kwao Shinyanga kwa matatizo ya Kifamilia,Chiku Kacka ametambulishwa juzi siku ya Jumatano na Mapacha watatu na Flolah Bambucha ambae ameuaga uongozi na hivi anakula upepo huko Dubai kwa mkataba mfupi,Ikumbukwe pia wanenguaji hao walitumika pia kama waitikiaji katika Bendi ya Taarab.

      Hapa wakiwa wameshiriki katika video ya wimbo mmojawapo wa Taarab.

 Juhudi za Kavasha Blog kutaka kuweka katika  mizania taarifa hii zilizaa matunda baada ya kumpata Katibu wa Bendi ya The Grand Utalii Ndugu Elibariki Zacharia Kunukula ambae pamoja na utangulizi huo hapo juu alikiri kuwepo na hali hiyo na kusema kuwa lengo hasa ni kuimarisha Bendi ya Utalii na pia kutengeneza maslahi na maisha bora kwa ujumla ya wanamuziki watakaobahatika  kuwepo kundini.
Alisema tumelazimika kuahirisha uzinduzi ili kupisha maboresho kwa kuwasimamisha kwa muda na kufanya zoezi la kuwapunguza wanamuziki kutoka 31 na kubaki na kundi dogo litakalokuwa na tija na baada ya hapo tutawarejesha wanenguaji.

                   Wakiwa katika pozi la muziki wa mwambao.

Kavasha ilimuuliza maswali machache zaidi kama ifuatavyo;
1.Kuna malalamiko kwa baadhi ya wanengu kuwa hawajui hatima yao na imebidi kwenda kujitafutia rizki kwenye majukwaa mengine,hili mnalisemaje kama Utalii Band?

Katibu wa Utalii Band anajibu-Hatujasema wazi kuwa tumeachachana nao,ukweli ni kwamba hatujaagana nao hivyo malalamiko yao hayako sahihi kama kuna aliyesimamishwa basi ni kwa muda na hapo kuna mawili ama tutamrudisha ama tutaagana nae kwa uzuri.

2.Mmoja wa wanenguaji wenu Chiku Kacka ametambulishwa na Band ya Mapacha watatu,nyie kama Utalii Band mna taarifa na mna kizuizi chochote juu yake?

Katibu wa Utalii Bandanajibu-Taarifa tunazo ila hatuwezi kuchukua hatua zozotemaana hakua mwajiriwa wetu,ndo kwanza tulikua kwenye mchakatowa kutoa ajira kwa wanamuziki na ndio lengo hasa la kusimamisha uzinduzi sambamba na kupunguza watu ili kuweza kuajiri.

3.Je unafikiri kuondoka kwake ni kwa ajira ya kujitafutia riziki?pengine mmewapumzisha bila malipo yoyoyte?

Katibu wa Utalii Band anajibu-Kwa kuwa ajira ilikua bado hivyo tulikua tukiwalipa kutokana na show hivyo kusimamishwa kazi mojakwa moja itasababisha muhusika kukosa malipo,binafsi naona yupo sahihi hata kama kuna mwingine amefanya hivyo ni sawa,avha watafute ridhika na sisi(Utalii Band tutakapokua tayari tutazungumza nao hukohuko walipo,hapo ni suala la makubaliano tu kwa maana hata wakati tunawachukua kuja Utalii Band hawakuwa majumbani mwao bali walikua katika kazi zao.

4.Unawazungumziaje wanamuziki hao waliosimamishwa kwa suala la nidhamu na uwajibikaji kazini?
Katibu Kunukula anajibu-Wapo v izuri kama ujuavyo kila mtu ana tabia yake lakini tunaishi kwa kuchukuliana maana hakuna binaadamu mkamilifu,Lakini kati yao huyu Chiku Kacka yupo vizuri zaidi maana anajitambua,anajituma na ana nidhamu ya hali ya juu kwa kweli kumkosa yeye ni pigo kwetu lakini naamini tutazungumza pale muda muafaka utakapofika.

5.Mnatarajia ajira kamili kuanza lini?
Katibu Kunukula anajibu-Tunatarajia kufanya hilo baada ya uchaguzi mkuu na tutazindua rasmi Januari Mwaka 2016.

Ndugu Elibariki Zacharia Kunukula,Katibu wa Bendi ya Grande Utalii tunakushukuru sana kwa ushirikiano,Kavasha Blog inatumaini kuwa ufafanuzi wako kwa suala hili utawaondolea sintofahamu wapenzi wa Le Grande Utalii na wapenda Burudani ya Muziki wa Dansi Nchini kwa ujumla.
AHSANTE SANA NA KARIBU TENA.

Baada ya hapo Kavasha blog ilifanya juhudi zakumtafuta mmoja  wa watajwa hapo anaetambulika kwa jina la Chiku Kasika ambae alikiri kuwa wameondolewa kwenye Bendi  hiyo kwa kile alichokisema maamuzi ya kumiza yaliyofanywa na uongozi wa Bendi hiyo kwani awali wenzake watatu waliondoka kwa ruhusa ya matatizo binafsi na baadae mmoja alionekana kwenye jukwaa la bendi nyingine na hapo ndipo ikawa chanzo cha kuondolewa  ghafla kwa wote waliobaki ambapo yeye alibahatika kujiunga na Mapacha watatu mwanzoni mwa wiki wiki hii.
  

Chiku Kasika ambae amechukuliwa na Mapacha Watatu.

 Ni matumaini ya wadau na wapenzi wa muziki kuwa hali hii itatengemaa na  Utalii Band kurudi katika kutoa burudani ileile walioizoea awali.