LATEST POSTS

Monday, August 17, 2015

ELIBARIKI ZACHARIA KUNUKULA;LE GRANDE UTALII BAND KUZINDUA ALBAM YAO MAPEMA SEPTEMBA.



                                                           MGENI WETU LEO HII

                   

                                         Mwanamuziki Elibariki Zacharia Kunukula.

Kwa mara nyingine Kavasha blog inakuletea mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi akiwa ni mtunzi,mwimbaji na mpiga kinanda kwa uwezo mkubwa kabisa,si mwingine bali ni Elibariki Zacharia Kunukula ambae tumeweza kuzungumza nae mengi yahusuyo familia yake,kazi yake ya muziki na mengine mengi yahusuyo tasnia hii,kwa ufupi kabisa nakuletea sehemu ya mahojiano hayo na mgeni wetu Elibariki ambae alianza kwa kujitambulisha;


     
                                                         Elibariki Zacharia Kunukula.                   

 Naitwa Elibariki Kunukula,ni mzaliwa wa Mkoa wa Singida katika kabila la Wanyiramba,alianza muziki mwaka 1998 Mjini Arusha na Bendi yake ya kwanza ilikua ikijulikana kwa jina la The Ambassadors Band,Muda si mrefu Bendi hiyo ilivunjika na nikaitwa Moshi kwenda kuanzisha Bendi iliyojulikana kwa jina la Rhino FM ambayo haikudumu na baade kutimkia Tanga nilipoalikwa kujiunga na Bendi ya Fax Jazz Band  ambapo nilidumu kwa muda mrefu sana nikifanya kazi na wakongwe kama vileSteven Hizza, Ziggy Saidi na Marehemu Hassan Ngoma Hawa ni wakongwe wa Bendi kongwe ya Mjini Tanga hapo zamani iliyojulikana kama ATOMIC JAZZ wakiwa pia  na Mzee Mganga ambaye ni Baba yake mzazi wa  Kassim Mganga huyu nyota wa Bongofleva hadi alipokuja Ally Choki kunichukua kujiunga na Extra Bongo ya Jijini Dar Es Salaam.
                  


                   
                                       Muimbaji wa Utalii Bendi ELIBARIKI  KUNUKULA.

Pale Extra Bongo sikukaa sana nikapata kazi kwenye mtandao wa Hotel ziitwazo Nyumbani Lounge Hotels & Resort zilizopo Tanga na Moshi mkoani Kilimanjaro nilipokua nikipiga  sequencer muziki wa mtu mmoja (jeshi la mtu mmoja) baada ya mkataba kwisha niliitwa na Profesa mmoja wa UDSM kuanzisha Bendi yake ambayo hakudumu kutokana na Profesa huyo kuwa hakujipanga ipasavyo kuanzisha Bendi,hapo ndipo nilipochukuliwa na Utalii nikiwa kama mtu wa sequencer baadae wakaja  Ramadhani Kilindi na Duncan ndumbaro wakanikuta nikipiga peke angu ndipo ulipoamua kuifanya kuwa Bendi hapo ndio mwanzo wa Utalii Bendi hii tuliyonayo sasa. 



                                                  Le Grande Utalii Band                                 

Bendi yetu inapiga nyimbo mchanganyiko,tunapiga kopi za aina zote kadiri tunavyozifanyia  mazoezi ingawa muziki aina ya Kavasha ndio kipaumbele chetu,pia tuna nyimbo zetu wenyewe tulizorekodi na zinapigwa redioni tumeshafanya video zake ambazo tutaziachia hivi karibuni.
Kuhusu albam tumejiandaa kuzindua albam yetu siku ya Tarehe 4 Septemba 2015  tunawaomba wapenzi wa muziki wa dansi  wote hususani  wa Utalii Band kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo kwani tumewaandalia mambo mazuri si ya kukosa kwa kweli.



                                        Elibariki (kulia)akiwajibika jukwaani.

Muziki mwingine aina ya Taarab unapigwa na kundi letu pacha la Utalii Bendi kwa maana kuwa kunakundi hili nililopo la muziki wa dansi linalojulikana kama Le Grande Utalii Band na hilo jingine linajulikana kama Utalii Taarab.

Suala la kuhamahama kiukweli linatokana na kutafuta maslahi na wakati mwingine ni kwa wanamuziki kushindwa kustahimili ukata pindi unapoingia kwenye Bendi Fulani.Na suluhisho la hili ni kwa Wamiliki wa Bendi kujiandaa vya kutosha kabla ya kuanzisha Bendi,pili ni kuwapa mikataba ya kueleweka ya ajira ya kueleweka kabla ya kuanzisha Bendi ili waache kututumikisha kama Big G ambayo ukiitoa dukani ni tamu lakini ukiitafuna baada ya muda inaisha utamu unaitema na kuitupa,Lakini pia yatupasa wanamuziki tujitambue kwani ujuzi wetu una thamani kubwa mno.



                              Kundi zima la Utalii Band wakiwajibika jukwaani.

Kuna baadhi ya Bendi hutoa mikataba naomba kwa kweli tuiheshimu mikataba hiyo ingawa wakati mwingine wamiliki wa Bendi hutoa mikataba minono wanapokuhitaji ila unapofika kwenye bendi husika hutekelezewi baadhi ya mahitaji muhimu yaliyoainishwa katika mkataba husika,na hata hali ikiwa hivyo unashindwa kuondoka kwa kuwa unalazimika kuilipa Bendi hali ya kuwa hujatimiziwa mahitaji yako lakini ulishasaini mkataba  na pesa ya kurudisha huna hapo unabaki na stress kibao hadi atokee tajiri mwengine akupe mkataba na pesa urudishe kule uende huku,unazunguka mule mule ingawa wengine wanashindwa kurudisha na kuzua tafrani.



Katika muziki nimepata mafanikio mengi sana ingawa sijapendelea kuyaweka wazi ispokua kikubwa ni kukuwa kwa kasi kubwa kwa kiwango change cha ujuzi wa muziki kwani tofauti na kuimba pia ni mpiga kinanda wa kiwango cha juu na hata Extra Bongo niliitwa kwa sababu ya kuwa mpiga Kinanda.

Le grande Utalii band inaundwa na wanamuziki wafuatao;

Waimbaji ni- 1.Elibariki Kunukula
                         2.James Mulamba na
                          3.Ramadhani Kilindi

Magitaa ni – 1.Omar Seseme-SOLO
                        2.Duncan Ndumbalo-RHYTHM
                         3.Juma Zegezo-Bass


Kinanda-Yupo Emma Mabele

Drums yupo   Steven Muzenga


                  
                                              Kundi la Utalii Bendi likifanya yao.

Awali tulikua na Komandoo Hamza Kalala ambaye kwa sasa amejipumzisha na huwa anakuja siku moja moja kutupa kampani,tulikua pia na Rashid Sumuni ambae kwa sasa ameondoka moja kwa moja.

Kundi la pili La Utalii Taarab lina wanamuziki wafuatao

Waimbaji wakiume ni-1.Mwinyimkuu
                                         2.Chai ya Rangi
                                         3.Melody Totoo

Waimbaji wa kike ni -1.Maina
                                       2.Poke
                                       3.Zulfa

Kinanda yupo- Moshi Hamisi Sentee

Drums yupo Fadhili.


                    
                                    Utanashati ni jambo la lazima kwa mwanamuziki anaejitambua.

Katika familia yetunaweza kusema ni familia ya muziki,wadogo zangu wote ni waimbaji ingawa kwa sasa wanaimba kwaya lakini kwa kiwango cha juu kabisa,Baba yangu nae alikuwa mwimbaji mzuri sana na alikuwa akifundisha kwaya ya Shuleni kwake kwani alikua ni Mwalimu,yeye nae alirithi kutoka kwa baba yake ambae alikua na kipaji kikubwa cha kuimba na kupiga zeze kwa ustadi wa hali ya juu.

                          
                                     akirekebisha vyombo ili mambo yaende vizuri

 Jambo kubwa ambalo siwezi kulisahau maishani ni kuondokewa na Baba yangu mzazi mzee Zacharia Kunukula mnamo Tarehe 23/05/2011 ambaye ukiachilia mbali ya  kifamilia lakini pia alikua mhimili wangu mkubwa kimuziki na alinisaidia sana kufika hapa nilipo.
Mwisho natoa ushauri kwa wanamuziki wenzangu tupendane,tushirikiane kwa kuyafanya haya tunaweza kkuirudisha hadhina heshima ya muziki wa dansi kurudi kama zamani na tuache kudharauliana kuwa huyu anajua na huyu hajui hapo hatujengi bali tunabomoa.
                       

                                   

                                                     Elibariki katika pozi.

Asante sana wana Kavasha kwa mahitaji ya kufahamu Bendi yako ya Utalii ilipo,inafanya nini nautaipata vipi kwa muda upi,ama kwa kunihitaji mimi mwenyewe kikazi zaidi ama kwa maelezo zaidi Wasiliana name Elibariki Zacharia Kunukula kwa;

 SIMU NAMBA +255715606171
EMAIL ADRESS-kunukulaelibariki@gmail.com


Kavasha Group inakupa pole kwa kuondokewa na Baba na nguzo yako Mzee     Zacharia Kunukula,tunaomba Mwenyezi Mungu amuweke mahali pema peponi Amen .

4 comments: