LATEST POSTS

Saturday, July 4, 2015

MFAHAMU MWANAMUZIKI TABU MAMBOSASA



Na Fredy Paschal

Habari yako dada Tabu Mambosasa, Wana Kavasha ndani na nje ya Nchi wangependa kujua machache kutoka kwako ili wapenzi wa muziki wa Dansi wapate kujua yale wasioyajua juu yako.


Swali 1.Ulizaliwa lini na wapi, vipi kuhusu familia?
Jibu-Nimezaliwa Katika Hospital ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam, natoka familia ya sanaa na michezo kwani kaka yangu ni Goalkeeper wa zamani wa Simba Marehemu Athuman Mambosasa, Baba yangu ni Msukuma wa Bukene Tabora na Mama ni mzaliwa wa Tabora mwenye asili ya Drc
Swali -2.Ni bendi gani ulizopitia na nafasi gani ulikua ukishiriki?
JIBU-Katika safari yangu ya Muziki nimepitia Bendi nyingi sana nikianzia katika Bendi ya International African Show Kwasakwasa nikiwa na Malik Star, Sisco Lunanga, Kwempa Lisasi na wengineo.Nilikua Dansa Sikinde, MK Group, Washirika Tanzania Stars, MCA International, Bana Maquis, Ngorongoro Heroes Band, Bantu Group na mwisho ni Double M sound.
Swali-3.Ni tukio gani usiloweza kulisahau katika safari yako ya muziki? JIBU-Tukio ambalo siwezi kulisahau katika maisha yangu ya muziki ni pale tuliposafiri na Bendi ya Bantu Group ilikua ziara ndefu sana.mwisho wa siku kila mmoja alirudi na njia yake. Swali-4.Nani alitoa mchango mkubwa hadi leo hii kuwa hapo ulipo?


JIBU-Katika watu waliotoa mchango mkubwa kuniwezesha kuwa hapa nilipo leo 

ni kwanza Comandoo Hamza Kalala, Pili ni Yuda Almasi, Tatu ni Yamamoto 

Bahati na mwisho lakini si kwa umuhimu ni Parmena Mahalu ambao wao 

wamenitoa katika kudansi hadi kuwa Muimbaji na mpiga Kinanda wa Kiwango cha juu.
Swali-5.Ni vikwazo gani unavyokumbana navyo katika safari yako ya kimuziki?


JIBU-Vikwazo ni vingi mno katika muziki na dawa ya kuvishinda ni subira, bidii 

na uvumilivu. Swali-6.Unadhani muziki wa dansi umepanda au umeshuka? Nini sababu? Muziki wa Dansi kwa sasa kiukweli umeshuka japo si sana tofauti na kipindi cha 

nyuma na sababu kubwa ni 1.Vyombo vya habari kutotoa sapoti kwa muziki wa 

Dansi badala yake vimejikita katka Bongo fleva tu
2.Sisi wanamuziki hatuna umoja maana bila umoja hakuna kitu 

kitakachotusaidia.


Swali-7.Je Ungependa watoto wako wafate nyayo zako? JIBU-Nisingependa watoto wangu wafuate nyayo zangu japo hili suala hutokea 

tu hasa kwa wao ambao wazazi wao wote ni Wanamuziki nikimaanisha mimi na 

mume wangu, hata hivyo mtoto wangu wa mwisho anaonekana kufuata nyayo 

zangu .


Swali-8.Nini Mafanikio yako katika uwepo wako katika tasnia ya muziki wa dansi?



Mafanikio yangu katika Muziki ni mengi ikiwa ni pamoja na kumiliki Bendi, 


kuitunza vema familia, na kupata mahali pa kujisitiri, mengine ni kujifunza 

mengi toka maeneo mbalimbali na watu mbalimbali nilipoenda na niliofanya 

nao kazi. Swali- 9.Jambo gani lililokukera katika maisha yako ya kimuziki? JIBU-Wakati nilipokua nikicheza show karibu kila Bendi haikuonesha kuthamini uwepo na mchango wa dansa maana tuliwekwa nyuma kwa kila jambo. Swali 10.Bendi gani hivi sasa unayofanyanayo kazi na vipi kuhusu 

masuala ya mkataba?

JIBU-Kwa sasa nina Bendi yangu ya Sequencer napiga Hotelini, Nina mkataba wa Kudumu katika Hotel ya Concord iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam, Karibuni sana napiga Jumatatu hadi Ijumaa. Swali-11.Nini Wito wako kwa wanamuziki wa sasa wa Dansi. JIBU-Wito wangu kwa wanamuziki wa sasa wa muziki wa Dansi tuwe na umoja kwani umoja na mshikamano ndivyo vitatutoa hapa tulipo.

Kavasha-Dada Tabu Mambosasa tunakushukuru kwa ushirikiano wako na tunakutakia kazi njema

TABU MAMBOSASA-Asanteni sana nanyie pia.


Tabu Mambosasa anapatikana kwa


namba:+255713 242 680


EMAIL:mambosasa4life@gmail.com

1 comment: