LATEST POSTS

Friday, February 26, 2016

MZEE MAPILI KUZIKWA LEO.

                                
                                  BURIANI MZEE MAPILI.


                                   Marehemu Sajenti Mstaafu Kasim Mapili.


Aliyekua gwiji wa muziki wa dansi Nchini Kassim Mapili aliyefariki usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano ya Tarehe 24 Februari 2016 anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu Jijini
Dar-Es Salaam.
          Akisalimiana na aliyekuwa Makamu wa Rais wa JM Ya Tanzania DK.Mohamed G.Bilali

Mzee Mapili wakati wa uhai wake alitumikia kwa muda mrefu Jeshi la polisi akiongoza pia Bendi ya Jeshi hilo yani Polisi Jazz akitunga vibao kadhaa vilivyoiweka juu Bendi hiyo kiasi cha kuleta upinzani kwa Bendi nyingine kama NUTA JAZZ,VIJANA JAZZ NK.
  Alikua mcheshi kwa kila mtu.

Mzee Mapili pia alipata kuongoza Chama cha Muziki wa Dansi Nchini CHAMUDATA na atakumbukwa kwa kupigania haki za Wanamuziki na kutaka mabadiliko kadha wa kadha ingawa alikutana na vikwazo vya hapa na pale.
           Mzee Kasim Mapili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa CHAMUDATA Ndugu Hassan Msumari na Kiongozi wa Mtandao wa Wanamuziki Nchini Anko John Kitime,msiba wa Marehemu Mzee Mapili upo Magomeni Mapipa mtaa wa Magomeni Nyumba namba 23 kwa mkwewe Bwana Wema ambae amemuoa mtoto wa Marehemu.

        Kwa hisia kali, kabisa akiwa jukwaani na Mjomba Band ya Mpoto.

Kavasha Group Tanzania itaendelea kuwapa Taarifa mbalimbali ikiwemo ya mazishi baadae.

Pia tunachukua fursa hii kuwapa pole wafiwa na tunamtakia malalo mema peponi,AMEN.
            Akiwa katika mazishi ya Fred Mosha siku moja kabla ya kifo chake.     

                            R.I.P MZEE KASSIM MAPILI.

0 comments:

Post a Comment