LATEST POSTS

Tuesday, February 23, 2016

HISTORIA YA MAREHEMU FRED MOSHA-BY WILLIAM KAIJAGE


                 HISTORIA YA FRED MOSHA …IMETAYARISHWA NA WILLIAM KAIJAGE
                  
                     Fredrick Camilius Mosha. 
KUZALIWA
 
• Fredrick Camilius Mosha alizaliwa tarehe 10-Feb-1979.
• Ni uzao wa baba mchaga (wa Kilimanjaro) na mama mnyakyusa (wa Mbeya).Ameoa na amejaaliwa kupata mtoto mmoja ambapo hadi anafariki alikua na umri wa miezi 7.


•Baba yake Fred Mosha marehemu Camilius Jerome Mosha alikuwa ndio mmiliki wa ukumbi wa White House uliokuwa Ubungo, ukumbi ambao bendi ya Marquis du Zaire (ambayo baadaye iliitwa Marquis Original) ulikuwa ndio ukumbi wao wa nyumbani.
•Mzee Camilius Mosha alifariki dunia tarehe 07-Jan-1990 (kipindi Fred akiwa kidato cha 1). Post ya mwisho ya Fred Mosha ilikuwa tarehe 07-Jan-2016 akikumbuka miaka 26 ya kifo cha baba yake. Baada ya hapo hakuandika post yoyote FB baada ya kuanza mihangaiko ya kwenda hospitali mbalimbali kwa ajili ya vipimo na matibabu.
•Mama yake, Bi Caroline Norbert, bado yu hai.


ELIMU NA WELEDI
•Fred alisomea shule ya msingi Wailes, shule ya secondary St Anthony (O-Level) na baadaye JKT Mgulani/Jitegemee (A-Level)
•Pamoja na kusoma elimu ya awali pamoja na kozi mbalimbali, Fred Mosha amesomea uandishi wa habari na kupata degree (shahada) kutoka chuo kikuu cha St Augustine (SAUT) kilichopo Mwanza.
•Alikuwa na weledi na vipaji vya mambo mengi ikiwemo weledi wa kuzijua lugha nyingi zikiwemo kifaransa na kilingala.

MAISHA YA NDOA
•Fred Mosha ameoana na Betha Fred. Hii picha ni siku walipofunga ndoa Jumamosi ya tarehe 31-Aug-2013 katika kanisa katoliki la Chang’ombe (Padri aliyewafungisha ndoa, alikuwepo pia kwenye misa ya mazishi ya Fred)
•Fred amejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume kama ilivyoelezwa juu aitwae Camilius(Jina la babu yake) ambaye hadi baba yake anafariki alikuwa na umri wa miezi 7.
                Siku ya ndoa na Bi Bertha            Mtoto Camilius                             

KAZI
•Kwa maisha yake yote, Fred Mosha amefanya kazi katika kituo cha radio cha Tumaini katika nafasi tofauti kutokea mwaka 1997.

MUZIKI WA DANSI
•Fred Mosha alikuwa ni mmoja ya wachambuzi bora kabisa wa muziki wa dansi ambao Tanzania imepata kuwa nao.
•Zaidi ya vipindi vya kawaida, ndani ya radio Tumaini alikuwa na vipindi maalum vya kila wiki vya kuchambua muziki wa dansi hususan kile cha kila Jumamosi kuanzia saa 5 hadi saa 7 mchana.
•Ameandika makala za muziki tokea alipokuwa shuleni. Kwa mfano alipata kuandika makala kuhusu Wenge Musica mwaka 1995 kipindi alipokuwa kidato cha 5 katika shule ya sekondari ya Jitegemee.
•Sambamba na mtafiti Frank Gunderson wa chuo kikuu cha Florida, USA, ameshiriki katika uandishi wa kitabu cha historia ya muziki wa dansi nchini ambacho kitakuwa cha kwanza cha aina yake nchini pale kitakapotoka.
•Ukiachia kuwa mtangazaji wa Tumaini Radio, makala zake nyingi za muziki zinapatika kwenye mitandao kadhaa ikiwemo georgem.co.tz, jambofestival.blogspot.com, Tumaini Media, wanamuzikiwatanzania na kadhalika.
•Makala nyingi zaidi ameandika katika makundi tofauti ya Facebook ambayo yanajadili muziki wa dansi.
•Zaidi ya uchambuzi, Fred Mosha pia alikuwa anajua kuimba na kupiga baadhi ya vyombo vya muziki. Alipokuwa mdogo, moja ya ndoto zake alipenda aje kuwa mwanamuziki. Ukaribu wa marehemu baba yake na marehemu Chinyama Chiaza (kiongozi wa bendi ya Marquis) ulimfanya aanze kufuatilia muziki akiwa na umri mdogo sana.

 Fred Mosha akiwa kazini wakati wa uhai wake.

UGONJWA NA KIFO
•Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2015, marehemu alianza kusumbuliwa na uvimbe mdogo shingoni. Uvimbe uliongezeka hadi kupelekea kwenda katika hospitali tofauti kuanzia Kairuki, Regency, Ocean Road na Muhimbili kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo kabla ya kugundulika kwamba alikuwa anaumwa ugonjwa wa saratani na baadaye kulazwa katika hospitali ya Muhimbili tarehe 06-Feb-2016    



•Amefariki dunia alfajiri ya Jumamosi 20-Feb-2016 katika hospitali ya Muhimbili. Amezikwa Jumatatu tarehe 22-Feb-2016 katika makaburi ya Kinondoni.
Bwana ametoa, bwana ametwaa. Jina la bwana lihimidiwe. Mungu amlaze mahali pema peponi.
Makaburini Kinondoni wanonekana hapa washirika wake wa karibu Ndugu Mbungiro Mayele,Ndugu Daudi Kisuguru,Mzee Juma Mbizo na Dada Tabu Mambosasa wakimsindikiza kwa mara ya mwisho.

                          R.I.P NDUGU YETU FREDRICK CAMILIUS MOSHA.

1 comment: