Pata vionjo vya Riwaya mpya katika maandalizi.
SHETANI KIAMBAZANI KWANGU-sehemu ya kwanza.Mtunzi/mwandishi,Lister Elia.
Nikiwa katika dimbwi la mawazo kutokana na mchakato uliotumika kuniengua kazini kwangu,kutokana na mmomonyoko wa uchumi wa dunia..., ghafla nainua paji la uso wangu ukutani.Nagundua kwamba mishale ya saa yangu ya ukutani,inanieleza ni saa nane na dakika thelathini na mbili za alfajiri.Hali nikiwa sina dalili yoyote ya usingizi,naamua kunyanyuka pale nilipokuwa nimeketi ili nijitengenezee kikombe cha kahawa,kuupasha mwili wangu joto kutokana na kinyuli cha alfajiri.
Kabla sijainuka,nahisi ufukuto fulani mithili ya mtokoto wa maji moto kwenye kiambaza karibu na sebuleni kwangu.Najaribu kupenyeza macho yangu nijue kulikoni?!..,sipati jawabu hivyo nanyanyuka niendelee na mkakati wangu wa "cha kahawa".
Napiga hatua ya kwanza,ya pili na ya tatu nikielekea jikoni,kufumba na kufumbua kope na mboni za macho yangu zinaanza kunicheza haraka haraka,kisa..nimekutana na kivuli...ITAENDELEA....
0 comments:
Post a Comment