LATEST POSTS

Friday, September 18, 2015

THE GRAND UTALII BAND YASIMAMISHA MADANSA WAKE WOTE

               THE GRAND UTALII BAND YASIMAMISHA WANENGUAJI WAKE.

        Waliokua wanenguaji wa Utalii Band wakiwa kazini kabla ya kusimamishwa.

 Bendi ya Utalii ya jijini Dar-Es-Salaam imewasimamisha kazi wanenguaji wake kwa wote kutokana na gharama za uendeshaji ambapo awali Bendi hiyo ilikua na makundi matatu ambayo ilikua ni The Grand Utalii A,The Grand Utalii B na The Grand Utalii Taarab,zoezi hilo litahusu kupunguza na wafanyakazi wa Bendi hizo na kuimarisha Bendi moja na ambayo itaweka mfumo wa ajira ya kudumu.

                Hapa ni mambo ya kusebeneka na Utalii Band.

Taarifa za awali zilizoifikia Kavasha Blog zilisema kuwa baadhi ya wanenguaji hao waliaga kwa matatizo ya kifamilia lakini walionekana kwenye majukwaa ya Bendi tofauti jambo lililoukera uongozi wa Grande Utalii Band na hivyo kuamua kuwatimua kazi,awali Bendi hiyo ilikua na wanenguaji sita ambao ni Chiku Kacka,Flolah Bambucha,Vero,Regina,Salma na Otilia Boniface,ambao kati yao inasemwa na chanzo chetu kuwa Otilia yupo na Bendi ya TOT katika kampeni,Regina na Salma wamerudi Double M Sound,Vero yupo kwao Shinyanga kwa matatizo ya Kifamilia,Chiku Kacka ametambulishwa juzi siku ya Jumatano na Mapacha watatu na Flolah Bambucha ambae ameuaga uongozi na hivi anakula upepo huko Dubai kwa mkataba mfupi,Ikumbukwe pia wanenguaji hao walitumika pia kama waitikiaji katika Bendi ya Taarab.

      Hapa wakiwa wameshiriki katika video ya wimbo mmojawapo wa Taarab.

 Juhudi za Kavasha Blog kutaka kuweka katika  mizania taarifa hii zilizaa matunda baada ya kumpata Katibu wa Bendi ya The Grand Utalii Ndugu Elibariki Zacharia Kunukula ambae pamoja na utangulizi huo hapo juu alikiri kuwepo na hali hiyo na kusema kuwa lengo hasa ni kuimarisha Bendi ya Utalii na pia kutengeneza maslahi na maisha bora kwa ujumla ya wanamuziki watakaobahatika  kuwepo kundini.
Alisema tumelazimika kuahirisha uzinduzi ili kupisha maboresho kwa kuwasimamisha kwa muda na kufanya zoezi la kuwapunguza wanamuziki kutoka 31 na kubaki na kundi dogo litakalokuwa na tija na baada ya hapo tutawarejesha wanenguaji.

                   Wakiwa katika pozi la muziki wa mwambao.

Kavasha ilimuuliza maswali machache zaidi kama ifuatavyo;
1.Kuna malalamiko kwa baadhi ya wanengu kuwa hawajui hatima yao na imebidi kwenda kujitafutia rizki kwenye majukwaa mengine,hili mnalisemaje kama Utalii Band?

Katibu wa Utalii Band anajibu-Hatujasema wazi kuwa tumeachachana nao,ukweli ni kwamba hatujaagana nao hivyo malalamiko yao hayako sahihi kama kuna aliyesimamishwa basi ni kwa muda na hapo kuna mawili ama tutamrudisha ama tutaagana nae kwa uzuri.

2.Mmoja wa wanenguaji wenu Chiku Kacka ametambulishwa na Band ya Mapacha watatu,nyie kama Utalii Band mna taarifa na mna kizuizi chochote juu yake?

Katibu wa Utalii Bandanajibu-Taarifa tunazo ila hatuwezi kuchukua hatua zozotemaana hakua mwajiriwa wetu,ndo kwanza tulikua kwenye mchakatowa kutoa ajira kwa wanamuziki na ndio lengo hasa la kusimamisha uzinduzi sambamba na kupunguza watu ili kuweza kuajiri.

3.Je unafikiri kuondoka kwake ni kwa ajira ya kujitafutia riziki?pengine mmewapumzisha bila malipo yoyoyte?

Katibu wa Utalii Band anajibu-Kwa kuwa ajira ilikua bado hivyo tulikua tukiwalipa kutokana na show hivyo kusimamishwa kazi mojakwa moja itasababisha muhusika kukosa malipo,binafsi naona yupo sahihi hata kama kuna mwingine amefanya hivyo ni sawa,avha watafute ridhika na sisi(Utalii Band tutakapokua tayari tutazungumza nao hukohuko walipo,hapo ni suala la makubaliano tu kwa maana hata wakati tunawachukua kuja Utalii Band hawakuwa majumbani mwao bali walikua katika kazi zao.

4.Unawazungumziaje wanamuziki hao waliosimamishwa kwa suala la nidhamu na uwajibikaji kazini?
Katibu Kunukula anajibu-Wapo v izuri kama ujuavyo kila mtu ana tabia yake lakini tunaishi kwa kuchukuliana maana hakuna binaadamu mkamilifu,Lakini kati yao huyu Chiku Kacka yupo vizuri zaidi maana anajitambua,anajituma na ana nidhamu ya hali ya juu kwa kweli kumkosa yeye ni pigo kwetu lakini naamini tutazungumza pale muda muafaka utakapofika.

5.Mnatarajia ajira kamili kuanza lini?
Katibu Kunukula anajibu-Tunatarajia kufanya hilo baada ya uchaguzi mkuu na tutazindua rasmi Januari Mwaka 2016.

Ndugu Elibariki Zacharia Kunukula,Katibu wa Bendi ya Grande Utalii tunakushukuru sana kwa ushirikiano,Kavasha Blog inatumaini kuwa ufafanuzi wako kwa suala hili utawaondolea sintofahamu wapenzi wa Le Grande Utalii na wapenda Burudani ya Muziki wa Dansi Nchini kwa ujumla.
AHSANTE SANA NA KARIBU TENA.

Baada ya hapo Kavasha blog ilifanya juhudi zakumtafuta mmoja  wa watajwa hapo anaetambulika kwa jina la Chiku Kasika ambae alikiri kuwa wameondolewa kwenye Bendi  hiyo kwa kile alichokisema maamuzi ya kumiza yaliyofanywa na uongozi wa Bendi hiyo kwani awali wenzake watatu waliondoka kwa ruhusa ya matatizo binafsi na baadae mmoja alionekana kwenye jukwaa la bendi nyingine na hapo ndipo ikawa chanzo cha kuondolewa  ghafla kwa wote waliobaki ambapo yeye alibahatika kujiunga na Mapacha watatu mwanzoni mwa wiki wiki hii.
  

Chiku Kasika ambae amechukuliwa na Mapacha Watatu.

 Ni matumaini ya wadau na wapenzi wa muziki kuwa hali hii itatengemaa na  Utalii Band kurudi katika kutoa burudani ileile walioizoea awali.

0 comments:

Post a Comment