LATEST POSTS

Friday, July 17, 2015

BANZA STONE KUZIKWA LEO SAA 10 ALASIRI



Na FREDY PASCHAL (KAVASHA GROUP TANZANIA)
Ramadhani A.Masanja"Banza Stone" kwa mujibu wa kaka yake Jabir alizaliwa tarehe 20/10 /1972.Alisoma katika shule ya msingi mnazi mmoja jijini dar,pia alipata elimu ya muziki katika jumba la utamaduni la watu wa korea.alipitia katika bendi ya african stars,TOT Bendi, Bambino Sound,Extra Bongo na kwa muda mfupi ktk Bendi ya Rungwe,atakumbukwa kwa tungo zake nzuri kama Hujafa Hujasifiwa,Mtu Pesa,Aungurumapo Simba 1&2,Kumekucha,Mtaji wa Masikini,Falsafa ya Mapenzi,Jahazi,Tushirikiane,Mpenzi toka ,Euro na nyingine nyingi,Banza alikua akiugua muda mrefu hadi jana tarehe 17/07/2015 alipotangulia mbele ya haki nyumbani kwake Sinza Kijiweni jirani na Vatican city,banza ameacha mtoto mmoja Hajji Ramadhan Masanja na anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam saa 10 alasiri.

"HAYA NI BAADHI YA MANENO YALIYOPO KATIKA WIMBO WA HUJAFA HUJASIFIWA".....Ningependa kujua baada ya kifo changu mimi Banza Stone watu watasema nini haapa duniani x 2 Basi namuomba Mungu anifanyie kama Yesu Masia alivyokufa baada ya siku tatu akafufuka lakini kwangu Banzastone mimi nasema haiwezekani ee, basi namuomba Mungu japo kwa sekunde moja ayafungue macho yangu na masikio yangu ili nipate kusikia watu watasema nini hapa duniani. Wengine utawasikia Banza anaimba sana, utawasikia oo Banza ni mzuri sana, utawasikia oo Banza anasauti nzuri, utawasikia oo Banza anatunga sana. Na wambea watachonga teeja hilo linavuta ngoma...."


INNA LIRAHI WAINAILLAHI RAJIUNI


0 comments:

Post a Comment