Ikiwa leo ni siku ya kukumbuka mashujaa wetu waliopigana katika vita vya Kagera dhidi ya majeshi ya uvamizi ya nduli Idd Amin Dada,Ukurasa huu wa Kavasha ulipata nafasi ya kuongea kwa ufupi na afande mstaafu na mwanamuziki nguli wa zamani wa Bendi ya Kimulimuli Mzee wetu Zahir Ally Zorro ambapo tuliweza kumuuliza maswali machache kama ifuatavyo;
Pichani:Mzee Zahir akipokea tuzo toka kwa Mhe;Jakaya Kikwete.
1.Nini ilikua dhima ya wimbo wako wa Tumerudi kishujaa?
Jibu-Ni wajibu mwema uliotekelezwa vyema,mashujaa walioanguka,mashujaa waliorudi,kwetu sisi askari ilikua kielelzo tosha kuhusu utekelezaji usio na shaka wa amri ya Amiri jeshi wetu mkuu wakati huo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambae mpaka kifo chake alisisitiza kuwa tutaenzi juhudi za mashujaa wetu milele.
2.Lini ilikua mwanzo kabisa kuimba wimbo huo hadharani?
Jibu-Ilikua mwezi wa August 1978 niliuimba kwanza mbele ya CDF wakati huo Gen David Musuguri ilikua Mgulani JKT ambapo alituelekeza tuurekodi haraka iwezekanavyo,tulitekeleza agizo lake na tuliurekodi.
3.Jeshi,Chama na Serikali waliupokeaje wimbo huo?
Jibu-Jeshi,Chama na Serikali vilifanya kazi kwa pamoja hivyo basi wimbo au kitu kikikubalika sehemu moja basi hakuna jinsi inakua kote imekubalika.
4.Hali ilikuaje kwa wananchi baada ya kuusikia wimbo huo?
Jibu-Tumerudi kishujaa ni wimbo wa wananchi,shurani nyingi zimetolewa kwa wanajeshi wa JWTZ,JKT,Magereza,Polisi na FFU ya Polisi na bila kusahau wanajeshi wa Mgambo na wananchi wa kawaida waliojitolea kwa hali na mali kuukata uvamizi.
''dikteta kakimbia na Uganda katuachia na vita tumeshinda''
PATA MANENO YA WIMBO ''TUMERUDI KISHUJAA''
Zahir; Tulikua tupo Arua wazazi wetu ee X2
Kwenye mipaka ya Uganda,na Nchi ya Sudan,
Kwenye mipaka ya Uganda na Nchi ya Zaire
Kwenye kijiji cha kobokoooo
Tukiwa tumemaliza kazi jukumu kubwa,mlotupa wetu wazazi kutoka Tanzania,kumfukuza msaliti,alovamia nchi yetu,na kumpa adhabu kisagondani ya mipaka yakeee.
Dikteta kakimbia na Uganda katuachia na vita tumeshinda ooo
Tulikua tupo Arua wazazi wetu ee
kwenye mipaka ya Uganda na Nchi ya Sudani,
kwenye mipaka ya Uganda,na Nchi ya Zaire
kwenye kijiji cha Koboko ,kijiji alichozaliwa fashist dikteta Idd Amin Dada oo
Ukatolewa mwito,wazazi munatwita wanenu,turudi nyumbani,
Makubaliano yakafanywa,mashujaa nusu wabaki,wakirekebisha mambo,
Tukiwa nusu tukaanza kufunga safari kurudi nyumbani
Tulipofika Kampala,tukaaga jamaa
Tulipofika Masaka,tukaaga jamaa,
Tulipofika mbarara,tukaaga jamaa
Tulipofika Kagera tukakuta wazazi wetuee,kwa vifijo na shangwe,wanenu kutupokeaaa
Wazazi pamoja na sisi wanenu tukageuza vichwaa,kuitazama Uganda,
Na kuwaacha mashujaa wetu,walopoteza maisha,ndani,ya nchi ya Waganda,walikufa kishujaa oohh
ooh wazazi
KIITIKIO; Wazaaazi,wazazi wetu eee
Wazaaazi,wazazi wetu eee
Mashujaa walokufa,wamekufa kishujaa,
Mashujaa tulorudi,tumerudi kishujaa,
Lengo na nia yetu wazazi ilikua moja,kuilinda ardhi yetu eee
kuilinda ardhi yetu eeeee X 2
Kipindi kilopita wazazi wetu ee
Kipindi kilopita wazazi,kilikua kigumu
Kile kipind cha vita wazazi kilikua kigumu ee
Katika muda mfupi,tumeweza kujua,
Nani kwetu ni rafiki,
Nani kwetu ni hasidi,
Yalopita si ndwele wazazi,tugange yanayokuja,
Umoja wenye nguvu,
Mshikamano wa dhati,
Na nidhamu za hali ya juu,kwa wanajeshi wetueee,
Ndio siri kubwa,ya ushindi wetu wazazi wetu ee,
Na yote kwa pamoja,
Ni matunda halisi,ya siasa safi nchini mwetu na uongozi boraa,
ooh wazazi
KIITIKIO; Wazaaazi,wazazi wetu eee
Wazaaazi,wazazi wetu eee
Mashujaa walokufa,wamekufa kishujaa,
Mashujaa tulorudi,tumerudi kishujaa,
Lengo na nia yetu wazazi ilikua moja,kuilinda ardhi yetu eee
kuilinda ardhi yetu eeeee X 2
0 comments:
Post a Comment