Leo hii Tarehe 7/7/2015,Wawakilishi wa kundi la KAVASHA wakiongozwa na Mlezi wa kundi hilo Ndugu Juma Kihenge akifatana na Wajumbe wa kundi la KAVASHA Tabu Mambosasa,Hamza Mapande na Alicom Tumaini walifika katika Hospitali ya Mkoa wa Kikanda wa Kinondoni ya Mwananyamala kumjulia hali Nyota wa muziki wa dansi nchini Ramadhani Ally Masanja maarufu Banza Stone.
Kutoka kushoto ni Hamza Mapande(KVS),Mama mdogo wa Banza,Jabir Masanja(kaka wa Banza),Tabu Mambosasa(Mhazini wa KVS)Mzee Juma Kihenge (Mlezi wa Kavasha) na Hamisi Masanja(kaka wa Banza).
Pamoja na kumjulia hali,wawakilishi hao wa KAVASHA GROUP TANZANIA pia waliwasilisha mchango wao kiasi cha Tshs 106,000/=kama pole kwa Banza Stone.
Akikabidhi fedha hizo kwa familia ya Banza Stone kwa mama mdogo wa Banza,mkuu wa msafara wa KAVASHA GROUP TANZANIA Ndugu Juma Kihenga alisema kundi lao lipo kwa ajili ya kusapoti Wanamuziki na tasnia ya muziki wa dansi kwa ujumla na kwa Banza ni sehemu tu ya mkakati wa kundi hilo,aidha amewasihi wadau wote kujitokeza kumsaidia kwa hali na mali Banza Stone kwani mchango wake kwa Tasnia ya muziki wa dansi ni mkubwa kwa wadau na kwa Taifa kwa ujumla.
Kutoka Kushoto ni Alicom ,mama mdogo wa Banza,Jabir Masanja,Tabu Mambosasa,MzeeJuma Kihenge na Hamisi Masanja.
Akiongea kwa niaba ya familia,Kaka wa Banza Stone Ndugu Jabir Masanja amesema anawashukuru sana wanakavasha wote kwa moyo wao waliouonesha kwa Ndugu yake na amewaomba mashabiki wengine wa Banza kuwaunga mkono katika kipindi hiki kigumu walichonacho.
Aidha Mweka Hazina wa KAVASHA Ndugu Tabu Mambosasa ameongeza kuwa hii ni mara ya pili kwa kundi hilo kumtembelea Banza Stone kwani mara ya kwanza walifanya hivyo walipomtembelea Banza nyumbani kwao Sinza na kutoa kiasi cha Tshs 103,000/= mwishoni mwa mwezi June.
PONGEZI KWA KUNDI LA KAVASHA,KUTOA NI MOYO SI UTAJIRI.
JIUNGE NA KAVASHA FACEBOOK ANDIKA
KAVASHA GROUP TANZANIA.
0 comments:
Post a Comment