LATEST POSTS

Saturday, July 16, 2016

KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA TANGU BANZA STONE AFARIKI DUNIA, IMEANDALIWA NA DAUDI KISUGURU.

NI MWAKA MMOJA SASA UMETIMIA TANGU TASNIA YA MUZIKI WA DANSI
IONDOKEWE NA MWANAMUZIKI NGULI
RAMADHANI MASANJA "BANZA STONE"
Mwanamuziki huyu alifariki mwaka mmoja uliopita yaani mwaka jana  2015
kabla ya kifo chake mitaani kulitokea fununu mithili ya mchezo wa kuigiza pale watu walipokuwa wakizusha habari ya kuwa amefariki.

Pamoja na uzushi huo habari hizo zilikuwa zikikanushwa na familia yake hata na yeye mwenyewe kwa mapenzi ya mola ijumaa ya tarehe 17/07/2015 hii haikuwa uzushi tena bali ya mungu yasemayo kila nafsi itaonja mauti ikatimia banza stone aliaga dunia akiwa nyumbani kwao sinza jijini dar es salaam
alipokuwa akiuguzwa na kuzikwa siku iliyofuata ambayo ilikuwa jumamosi ya tarehe 18/07/2015 katika makaburi ya sinza kifo chake inasemekana kilitokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya ubongo.

Ramadhani Masanja alimaarufu banza stone alizaliwa jijini dar es salaam tarehe 20/10/1972 akiwa mtoto wa tisa kati ya watoto kumi na moja ,alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi MNAZI MMOJA ya hapahapa jijini dar es salaam ambako alianza darasa la kwanza mwaka 1981 na kuhitimu darasa la saba mwaka 1987 ,mara baada ya kumaliza shule ndipo alipoanza kujishughulisha na mambo ya muziki lakini akianza na muziki wa Hip hop enzi hizo ulikuwa ukisikilizwa kwenye radio tu akiwa na wenzake kama K - ONE na SCOS MAN hiyo ilikuwa mwaka 1989.

Mwaka 1990 akaanza mchakato mpya wa kunengua muziki wa dansi wa enzi hizo za miaka hiyo ya 1990 ambayo miziki ya congo ndiyo ilikuwa imetawala
"kwasakwasa" ,"nzawisa" n.k.

Walikuwa wakicheza sana kwenye maharusi yeye pamoja na wenzake YELLOW MAN na JESCA ONGALA mtoto wa DR REMMY.
Baada ya hii kuona hailipi ndipo alipoamua kujifunza muziki katika kituo cha utamaduni cha watu wa korea alikopelekwa na jirani yao aitwaye MZEE KAPIZO na kujifunza kupiga drums na bendi yake ya kwanza ilikuwa THE HEART STRINGS ,TWIGA ,AFRI - SWEZI na baadae akajiunga na ACHIGO BAND katika hizi alikuwa hamalizi hata mwaka ni miezi sita anaondoka.

Mnamo mwaka 1995 ndipo alitua THE AFRICAN STARS BAND wana twanga pepeta ikiwa bado changa kabisa ikiwa na mwaka mmoja tangu ianzishwe na kufanikiwa kurekodi nao albamu ya "kisa cha mpemba"sasa akiwa kama muimbaji.

Alihudumu ndani ya twanga pepeta kwa muda wa miaka mitano na kuachana nayo mwaka 2000 Banza stone aliihama african stars na kujiunga na TANZANIA ONE THEATRE ( T O T ). Wana achimenengule iliyokuwa ikiongozwa na KAPTENI JOHN KOMBA ambaye kwa sasa nae ni marehemu na kuweza kutunga nyimbo kama "mtaji wa masikini","elimu ya mjinga", akiwa hapa aliwahi kupata mafunzo ya muziki katika chuo cha sanaa bagamoyo. 

Mwaka 2003 aliachana na T.O.T. na kuanzisha bendi yake iliyokuwa ikifahamika kama BAMBINO SOUND bendi ambayo ilitoka na kibao matata kisemacho "miye niseme na wewe useme nani atamsikiliza mwenzie" kwa bahati mbaya bendi hii haikudumu ikasambaratika na yeye kurejea tena AFRICAN STARS  na baadae akajiunga na EXTRA BONGO, TWANGA CHIPOLOPOLO,
RUFITA JAZZ BAND.

Mwaka huo huo wa 2003 Banza alikuwa ni miongoni mwa wamuziki watatu walioshiriki kwenye zing zong iliyoandaliwa na mfadhili aitwaye MOHAMED MPAKANJIA mwingine ni ALLY CHOKI na MWINJUMA MUUMINI .
tutaendelea kumkumbuka kwa nyimbo zake zilizoibamba jamii enzi za uhai wake
kama "mtaji wa masikini" ,"elimu ya mjinga" ,"aungurumapo simba" ,"mtenda akitendewa" ,"falsafa ya maisha" ,"kumekucha" ,"mimi niseme nawe useme" ,"mshenga" na "sema unachotaka"

MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI NA AMPUNGUZIE ADHABU ZA KABURI - AMIN.

0 comments:

Post a Comment