LATEST POSTS

Sunday, September 13, 2015

MASHUJAA BAND YAWAPAGAWISHA WAKAZI WA LINDI KATIKA HAPO JANA NDANI YA PEACE BEACH HOTEL


      MASHUJAA BAND YAPAGAWISHA WAKAZI WA LINDI                                HAPO JANA SEPT 12-2015.
              


                                                               
                  


Siku ya Jumamosi 12 Septemba 2015,Bendi ya Mashujaa ilifanya onesho la kufana katika Hotel ya Peace Beach Mjini Lindi na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Mjini humu.
Kwa ufupi mambo yalikua kama hivi-Saa 21:30 Wapiga ala wakiongozwa na Baba Isaya na Freddy Masimango walianza kupasha ala zao moto hadi pale Saa 22:30 Raja Ladha alipokuja kuendeleza harakati kwa machombezo anuwai hadi saa 23:05 pale Mirinda Nyeusi alipofika kuongezea yake ambapo aliweka hadharani nyimbo mpya mbili zenye utamu wa aina yake Mama wa Kambo na Magdalena ambao una midundo flani amazing ya kiasili ambao ulionekana kuwakuna mashabiki vilivyo.

                 

Mambo yalikua tele ama kwa hakika kwani muda si mrefu majira ya Saa 23:20 Kundi la wasanii wa Bongo Movie likiongozwa na Mwenyekiti wa ‘’Mama Sema na mwanao’’ Steven Mengele ‘’Steve Nyerere maarufu kama Tajiri Mfupi ama Tajiri mbishi nao walitinga maeneo ya kiota hicho cha burudani wakiwa pamoja na Odama,Wastara,Maya,Chuchu Hansi  nk amabao waliungana na Wema Sepetu na Petit Man Wakuache ambao waliingia mapema zaidi.
         

Chombezo linaendelea ambapo Patient Buddas anapanda jukwaani kuungana na Raja Ladha na kutelemsha kitu murua ambacho ni kopi ya Werrason Ngiama Makanda hadi pale saa 23:50 amabapo programu ya Bendi inaanza rasmi Charz Baba,Jado FFU wanaingia na kushusha vibao mfululizo wakianza na Mama Kibonge,Safari yenye vikwazo,Deodata ambao Raja Ladha aliutendea haki hasa na katika wimbo huo ndipo timu ya wacheza show ilipoibuka na kuongeza shangwe kwa mashabiki ambao hawakutaka kabisa kukatizwa kwa Sebene wao walitaka ‘’kuchinja bata tu’’
                   


Kuanzia Saa 01:30 kwa Nusu saa nzima aliamua kuwapagawisha mashabiki kwa machombezo mseto ya baikoko na Mchiriku ambapo vipande vya naipenda Simba na Naipenda Yanga mshabiki wa damu viliwapagawisha mashabiki wa timu husika pale inapotajwa timu yao ambao mambo ya dau la Mtani Jembe yalionekana kuchukua nafasi hadi pale alipowatuliza kwa Wimbo wake maarufu wa Risasi Kidole ambapo Rapa Bora mara nyingi mfululizo Saulo Fergusson nae aliibuka kuja kufanya yake,ikafata Mama mimi nashangaa wimbo utunzi wa Mirinda Nyeusi ambalo ni Rhumba la ukweli.

Saa 02:30 Steve Nyerere anakaribishwa kwa nyakati tofauti pamoja nae Wastara kuja kusalimia kisanii ambapo alijaribu kupita walipopita mastaa mwisho akatoka nje kidogo ya mstari pale alipotoa za aliselema kitu kilichoibua mitizamo ya kiitikadi ambapo kwa haraka Meneja wa Bendi ya Mashujaa Martin Sospeter aliwahi kurekebisha na programu ikaendelea hadi mwisho.

TATHMINI YA ONYESHO

1.MAHUDHURIO-Ilianza kwa uchache lakini kufika katikati ya onesho Ukumbi ulijaa sana.

2.HALI YA JUKWAA-Iliathiri ufatiliaji kwa wahudhuriaji walioketi kwani hawakuweza kuona mbele pale wenzao wanapoamka na kwenda kucheza kwani eneo la jukwaa limeinuliwa kwa sentimeta chache sana kutoka chini.






3.NISHATI YA UMEME- Hali ya kuungua na kuongezeka kwa umeme ilionekana kuwa tishio kwa onesho kama sio juhudi za wahusika wa Bendi na Hoteli wa kutumia jenereta moja kwa moja bila kujali uwepo wa umeme.

4.HALI YA BENDI-Bendi ilikua katika hali nzuri na walikua katika morali ya kufanya kazi ingawa baadhi ya waliohudhuri walihoji kutokuwepo kwa Nguli Elistone Angai ambapo inasemwa ataungana na wenzake leo katika onesho lao la pili katika Wilaya ya Nachingwea,Mwingine ambae hakuwepo ni Rapa Sauti ya Radi ambae haijajulikana anamatatizo gani.
                   

5.NYOTA WA ONESHO-Karibia wote walijitahidi kwa kadiri ya uwezo wao,ala zilikung’utwa vizuri ila Kinanda cha Freddy kilikua habari ya show,aidha Charz Baba,Mirinda na Raja Ladha ilikua siku yao.

                     
6.UMALIZIAJI WA ONESHO-Kabla ya wimbo wa Mwisho nadhani hakukuwa na mawasiliano mazuri kwani baadhi ya wapigaji walikwisha weka vifaa chini na hata ulipoongozwa wimbo huo haikuwezekana na huo ndio ukawa mwisho wa show hiyo.

Wito- kuwe na mawasiliano mazuri katika kumalizia show kwani kunawafanya watu waondoke na hamu yao kulikoni kuwaondoa na sintofahamu kama ilivyokua.Kwa asilimia 95% show ilikua nzuri sana kulinganisha na maonesho kadhaa ya Mashujaa ambayo nimepata kuyahudhuria na hata kwa maoni ya wengine waliohudhuria akiwepo mmiliki wa duka la Hadjis Fashion Ndugu Hadji Chaula ambae amesema onesho hilo ni la ukweli kuliko lile lililofanyika awali Mjini hapa.

TAKE HOME-Meneja wa Bendi hiyo Ndugu Martin Sospeter amedokeza kuwa Bendi hiyo itaweka kambi kwa muda wa wiki mbili Mjini hapa kwa ajili ya maandalizi ya vibao vyao vipya vinavyotarajiwa kuwa moto wa kuotea mbali.


 KILA LA HERI WAZEE WA KIBEGA MASHUJAA  BAND.


0 comments:

Post a Comment