KAVASHA BLOG.
Inakuletea wimbo uliopata kutamba wakati wa uhai wa Bendi maarufu mjini
Iringa na nchini kwa ujumla yani Tancut Almas Orchestra uitwao Butinini,ikiwa na wanamuziki weengi maarufu akiwemo mwenyewe mtunzi wa wimbo huu Kasaloo Kyanga,Kyanga Songa,Kalala Mbwembwe,John Kitime nk ikihanikiza kwa vibao mbalimbali vingine katika anga hili la muziki wa dansi nchi kama vile Masafa marefu,Lutandila,Urafiki wa uongo nk.Wimbo huu aliutunga mahususi kwa ajili ya mkewe Jane Butini aliekuwa akicheza Netiboli Timu ya NBC ambaye ni Ndugu wa Mwanasoka wa zamani wa klabu ya Reli ya Mjini Morogoro kiboko ya vigogo wakati huo Dancun Butinini,Jane baadae alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
.JANE BUTININI
BENDI-TANCUT ALMAS ORCHESTRA
MTUNZI-KASALOO KYANGA
MTINDO-MANGALA DANSI.
Kasaloo-Nimepatwa na wasiwasi mwingi moyoni
Maana naona maadui wengi wananifatata
Wanataka kuvvuruga penzi letu na mamaee
Kasaloo-Nimekuchagua........
Wote-Ni weweee Butinini
Kasaloo-Uwe wa Maisha
Wote-Mileleee mpaka kufaa X2
WOTE-Sintokwacha mamaaaa Butinini hata wasemee vipi X 4
MAREHEMU KASALOO KYANGA NA MKEWE JANE BUTININI
KIITIKIO
Kilichobaki nizibe masikiooo,nifunge na macho,
Maana sitaki kusikia cha mtu wala kuona,
Mwingine zaidi yako wewee.....Butinini X2
Kasaloo-Butinini nimekuchagua
wewe mama
Wote -Butininiii
Kasaloo- Jane Butinini wapete na kidole mama
Wote - Butininii
Kasaloo- Jane Butinini wa kufa na kupona mamaee
Wote - Butinini
Kasaloo- Ohh Butinini nimekuchagua wewe mama
Wote -Butininiiii
Kasaloo-Ooh Butini wa kufa na kuzikana mamaee
Wote - Butini
Kasalo- Ooh Butinini wa pete na kidole mamaee
Wote - Butininiii
Kasaloo- Butinini ya malaika mamaee
RUDIA KIITIKIO
Kilichobaki nizibe masikioo nifunge na macho,
Maana sitaki kusikia cha mtu wala kuona,
Mwingine zaidi yako wewe,Butinini X2
Fimboooo lugodaa
Fimboooo lugodaa
.KASALOO JUNIOR MTOTO WA KASALOO NA J BUTININI
0 comments:
Post a Comment