LATEST POSTS

Sunday, August 2, 2015

MAZISHI YA BABA WA ANKO JOHN KITIME KUFANYIKA JUMANNE TAR 4/8/2015 MKOANI IRINGA.





                   
                         MAREHEMU MZEE FRANCIS KITIME WAKATI WA UHAI WAKE.


Mazishi ya Baba wa Mwanamuziki Nguli wa Dansi nchini John Kitime,Mzee Francis Kitime yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne Mkoani kwao Iringa.

Akiongea na KavashaBlog,Anko John Kitime amesema kuwa Baba yake alifariki usiku wa kuamkia Jumamosi ya Tarehe 1/8/2015  Saa Saba na nusu usiku katika Hospitali ya Muhimbili alipokua amelazwa baada ya kuugua.



ANKO JOHN KITIME AKIWA NA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI MSIBANI NYUMBANI                                   KWAKE SINZA JIJINI DAR-ES-SALAAM.

Anko Kitime ameongeza kuwa Siku ya Kesho Jumatatu Saa Nne Asubuhi kutakua na Misa na kuaga mwili wa Marehemu katika hospitali ya Muhimbili ambapo itafatiwa na safari ya kuelekea Mkoani Iringa kwa ajili ya Mazishi yanayotarajiwa kufanyika Siku ya Jumanne Tarehe 4/8/2015.

KATIBU WA KAVASHA GROUP TZ JOHN SHEKWAVI(MWENYE SHATI JEUPE)AKIWA NA WANAMUZIKI SAIMON MWAMKINGA,BENNY OMARY,MZEE MASAMBA PAMOJA NA NDUGU NA JAMAA NA MARAFIKI WALIOFIKA MSIBANI NYUMBANI KWA ANKO KITIME SINZA DSM.

Group Tanzania inatoa pole nyingi kwa Ndugu,Jamaa na marafiki wa Mzee Francis Kitime kwa kuondokewa na muhimili nguzo hiyo muhimu ya familia,sote tunamuombea malazi mema peponi Amen.

                       
        
              

              PICHA YA KUSHOTO NI WANAMUZIKI BENNY OMARI NA MZEE            MASAMBA,PICHA YA KULIA NI VIONGOZI WA KAVASHA GROUP,KATIBU J SHEKWAVI NA MWEKA HAZINA TABU MAMBOSASA WAKIKABIDHI UBANI WAO KWA  ANKO J KITIME KUTOKA KWA WANACHAMA WA KAVASHA NCHINI.                                                                     

                       

                                BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA,
                 
      ROHO YA MAREHEMU MZEE FRANCIS KITIME IPUMZISHWE KWA AMANI

                                                             AMEN.













0 comments:

Post a Comment